Unapotaka kuingia chooni ,litangulize guu lako la kushoto na wakati wa kutoka litangulize guu la kulia. Usichukue kitu ambacho kinajina la Mwenye-ezi-mngu au Mtume (s.a.w) wala usiingie pasina viatu wala kichwa wazi.

Na useme wakati wa kuingia chooni:-

(Bismillah, A-udhubillah minarrijsi nnajisi al-khabithi al mukhbithi al-shetani)

(MAANA YAKE: Kwa jina la Mwenye-ezi-mngu ,najirinda kwa Mwenye-ezi-mngu najilinda na shetani (majina al-najisi na mengineyo yote yanamhuhusu shetani).

Na usome ;-

(Allahuma inny audhubika minal-khubuthi wal khabaithi).
(MAANA YAKE;- Ee, Mola hakika yangu najilinda kwako na mashetani wabaya ,waume na Wake).

Na wakati Ukitoka Chooni Soma:--

(Ghufranaka Al-hamdu-lillahilladhi adhhaba anny mayu-udhiny wa abqa alayya ma yanfauny)
MAANA YAKE;--- Naomba msamaha kwako wewe -Ninamuhimidi Mngu ambaye ameniondolea Mimi ambacho kinaniudhi na akanibakishia ambacho kinanifaa.

Na inatakikana ajiandalie na maji au mawe kabla hajaingia chooni. Na vilevile inatakikana ajilinde na najisi kama alivyosema Mtume (S.A.W):--

(HAKIKA KUENEA KWA ADHABU YA KABURI NI KUTOKAMANA NA NAJISI. BHASI NI JUU YAKE MTU KUJIHIFADHI VIZURI).