Na tumeteremsha kutoka mbinguni Maji yaliyo twahara.
Hakika Mwenye-ezi-Mngu anawapenda wenye Kutubia na anawapenda wenye kujitahrisha.
Ugunguo wa SALA ni TWAHARA.
MAJI YAFAAYO KWA TWAHARA
Maji ambayo yafaa kujitahirisha ni namna sabaa:-
1)Maji ya Mvua
2)Maji Bahari
3)Maji ya Mto
4)Maji ya Kisima
5)Maji ya Chem chem
6)Maji ya Barafu
7)Maji ya Mmande.
Haifai kuonfoa hadathi wala najisi ila kwa Maji mutlaq (yasiwe yanaitwa kwa jina jengine kama Maji ya marashi na mengineyo).
Maji ni ya namna mbili huwa ni Qullateni na yasiyofikilia Qullateni. Maji ya Qullateni hayaharibiki kutawadhaa au kuoga janaba ndani yake .Yasiokuwa Qullateni haifai kujitahirishia ndani yake.
0 Comments