DAMU - Hutoka katika tupu ,ni Damu tatu;-
(1) Heydhi
(2) Nifasi
(3) Ugonjwa

DAMU YA HEYDHI
Hutoka kwenye tupu ya Mwanamke Kwa njia ya uzima pasina sababu ya Kuzaa.

DAMU YA NIFASI
Hutoka baada ya kuzaa.

DAMU YA UGONJWA
Hutoka katika siku zisizokuwa katika siku za Heydhi wala Nifasi.

Uchache wa zama za kuingia Hedhini mwanamke ni mchana na usiku (saa 24). Na wingi wake ni siku kumi na tano (masaa 360). Na ghalibu ni siku sita au saba (baina ya masaa 144 na 168).

Na uchache wa kuingia damu ya nifasi (kuzaa) ni kitambo na wingi wake ni siku sitini na ghalibu ni siku arubaini.

Na uchache wa kutahirika kati ya hedhi mbili ni siku kumi na tano wala hapana mwisho wa wingi huo. Na uchache wa zama ambazo huingia hedhini mwanamke ni miaka 9 ; na uchache wa mimba ni miezi sita na wingi wake ni miaka minane na ghalibu ni miezi tisa.