Kila kilicho maji maji na kinachotoka kwenye tupu mbili ni Najisi isipokua manii.

Mkojo na choo - ni wajibu kuziosha isipokua mkojo wa mtoto wa kiume asiyekula chakula ila maziwa - hutahirika kwa kunyunyiza maji juu yake.

Wala haisemehewi kitu mingoni mwa najisi ila uchache wa damu, usaha na mnyama ambaye hana damu yenye kuturuzika kama nzi, tungu, na mfano wa hawa, atakapoingia katika chombo akafariki ndani yake. Hakika yeye HANASIJISHI.

Hayawani wote ni Tahara isipokua Mbwa na Nguruwe na wenye kuzaliana na hawa wawili au mmoja wapo, Mfu wote ni najisi ila mfu wa samaki na nzige (parare) na Mwanadamu.

Huoshwa chombo chenye kunajisishwa ni mbwa na nguruwe mara saba. Mara moja hutungamanishwa ni Mchanga na huoshwa baki za najisi nyengine mara moja na mara tatu ni bora zaidi.

Na wakati likibadilika tembo kwa nafsi yake huwa ni tahara na likibadilika kwa kutiwa kitu ndani yake halitahiriki.